Jumatano, 20 Agosti 2014

EBOLA::POLISI WAVUNJA MAANDAMANO NCHINI LIBERIA Maafisa wa usalama wakiwa Westpoint baada ya uvamizi wa kituo cha EbolaPolisi nchini Liberia wamerusha vitoa machozi kuwatawanya umati uliojaa hasiria katika mji mkuu Monrovia wakipinga kuzingirwa kwakitongoji chao na maafisa wa Usalama.Maafisa wa usalama walilazimika kutumia nguvu baada ya waandamanaji kuanza kuwapura kwa mawe katika kitongoji cha Westpoint .Awali rais Ellen Johnson Sirleaf alikuwa ametangaza hali ya tahadhari na amri ya kutotoka nje kwa wenyeji wa vitongoji hivyo vilivyoathirika na ugonjwa wa Ebola.uliokuwa ukiandamana kupinga kuzingirwa kwa eneo wanakoishi kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa ebolaWalioshuhudia walisema kuwa vikosi vya usalama vilivyotumwa kuzuia kutembea kwa watu baada ya kituo cha afya kuvamiwa wiki iliyopita viliwaudhi watu ambao walijipata hawana tena uhuru wa kutoka maeneo hayo ya Westpoint.Wahudumu wa Afya wakipuliza dawa ya kuzuia kuenea kwa EbolaRais Sirleaf alikuwa ametangaza amri ya kutotoka nje nyakati za usiku kuanzia saa tatu hadi saa kumna mbili asubuhi.kufuatia amri hiyo Watu hawakuruhusiwa kuingia au kutoka nje ya eneo la kitongoji cha West Point viungani mwa jiji la Monrovia.Aidha, eneo fulani katika mji mkuu wa Monrovia litatengwa katika harakati za kuthibiti kuenea kwa ugonjwa hatari wa Ebola.Watu waliojawa na hamaki walishambulia kituo cha afya katika eneo la West Point siku ya Jumamosi, na kupelekea kutoroka kwa wagonjwa 17 wa Ebola.Rais Sirleaf amelaumu serikali yake kwa kutothibiti homa hiyo ya Ebola, kwani haikufanya vya kutosha kuboresha hali ya maisha ya raia walipopuuza ushauri wa wafanyakazi wa huduma za afya na kutotilia maanani tahadhari rasmi za Ebola.Hata baada ya Liberia kutangaza hali ya dharura kufuatia mlipuko waEbola mapema mwezi huu, ugonjwahuo unazidi kusababisha vifo nchinihumo.Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleafatangaza amri ya kutotoka nje .Ebola haina tiba lakini Shirika la Afya Duniani (WHO) liliidhinisha matumizi ya dawa zilizokuwa zikifanyiwa utafiti kufuatia mlipuko mkubwa wa Ebola Afrika Magharibi.Kwa mujibu wa waziri wa maswala ya habari wa Liberia, Lewis Brown, madaktari watatu walioambukizwa Ebola wakiwahudumia wagonjwa wa Ebola, wameonyesha dalili za kuimarika kiafya, baada ya kutumia dawa zilizokuwa zikifanyiwa majaribio juma lililopita.Watu 1,229 wameripotiwa kufarika katika kanda ya Magharibi mwa Afrika tangu ugonjwa huo uzuke miezi minne iliyopita.Ebola husambazwa moja kwa moja kupitia maji maji ya mwili ya waliougua .

Jumanne, 19 Agosti 2014

MWANDISHI WA HABARI AUWAWA.. James Foley enzi za uhai wake akiwana vitendea kazi vyake.Kikosi cha kiislam cha kijeshi chenye msimamo mkali kimeachiliavideo inayoonesha mauaji ya mwandishi habari mwenye asili ya Marekani. James Foley alipotea tangu alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria miaka miwili iliyopita na sasa ameuawa.Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo ,serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwanini James Foley auawe.Katika mtandao wa kijamii wa Facebook familia ya mwandishi huyo iliandika kuwa’tunajua kwamba wengi wenu mnasubiri uthibitisho ama majibu ya maswali yenu,tafadhalini muwe watulivu mpaka nasi sote tupate taarifa tunazo tamia,na tunaomba muendelee kumbumbuka Foleys na kumwombea kila siku.’’Katika video hiyo iliyobeba ujumbe unaosomeka kua ujumbe kwa Marekani,mwandishi huyo pia alionekana akiwa chini ya ulinzi wa mtu aliyekua amevalia kinyago usoni,askari huyo alikua aku akizungumza ndani ya lafidhi yenye athari za Uingereza,akisema kua kifo cha mwandishi huyo ni matokeo ya mashambulizi ya magurunedi yalowalenga wa Iraq.

Wakati unapumzika baada ya michakoto ya maisha..pumzika kwa kuangalia KICHOGO YOUTUBE

https://www.youtube.com/watch?v=fMmDSHexcIg&feature=youtube_gdata_player

DIRECTOR MDOGO WA FILM ZA KITANZANIA MDOGO KULIKO MADIRECTOR WOTE,,,ANAYE KUJA JUU KATIKA TASNIA YA FILAMU FADHILI MANDEPE ANAYE TAMBA NA FILM ZAKE KAMA VILE KICHOGO,SIKITIKO NA POWER OF GOD AMBAYO IPO MBIONI KUTOKA....AWAOMBA WATANZANIA KUKAA MKAO WA KUPAKUA NA KULA....TAZAMA FILM YAKE YA KICHOGO..BONYEZA HAPA YOUTUBE....

https://www.youtube.com/watch?v=fMmDSHexcIg&feature=youtube_gdata_player

Jumatano, 13 Agosti 2014