Jumatatu, 30 Juni 2014
USA KUONGEZA WANAJESHI 200 IRAQ... USA kuongeza vikosi Baghdad kutokana na Tisho la kundi la wapiganaji wa ISISRais Barak Obama ametangaza kuwa anatuma vikosi 200 zaidi , na pia helikopta zisizoKuwa na ruban nchini Iraq.Katika barua yake wa baraza la Cogress rais Obama amesema kuwa vikosi hivyo vitatoa msaada wa nyongeza na usala kwa ubalozi mjini Baghdad.Rais Obama amesema vikosi hivyo vya ziada vimepewa mafunzo kabambe ya kijeshi na majukumu yao makuu yatakuwa kuwalinda raiawa Marekani na mali zao huko Iraq.Wataungana na wanajeshi wengine wa Marekani walioko Badghad wanaolinda ubalozi wa Marekani.Katika barua yake kwa bunge la Congress, Obama amaesema amepeleka pia helicopters,na ndegezisizo na rubani kuimarisha ulinzi huo.Tayari Marekani washapeleka washauri wakijeshi wapatao 180 kufanya kazi na jeshi la Iraq.Obama kupeleka pia ndege za kivita zisizo na rubani 'drones' huko BaghdadHata hivyo idadi ya jumla ya wanajeshi wa Marekani nchini Iraq ni kama 750 pekee.Huku mapigano yakiendelea kuchacha huko Iraq rais Obama amesisitiza hatapeleka majeshi ya ardhini nchini lakini hatua ya kufanya mashambulizi ya angani dhidi ya kundi la wapiganaji wa ISIS huenda ikachukuliwa.Wakati huohuo Balozi wa Saudi Arabia katika umoja wa mataifa amekana madai ya Waziri mkuu wa Iraq , Nouri Maliki kwamba nchi yake inatoa usidizi wowote kwa kundi la ISIS na pia kupinga nadharia kuwa usaidizi wa Saudia kwa waasi wa Syriaumechangia kuliinua kundi hilo la ISIS.Tangazo la kundi hilo la ISIS hapo jana kwamba wataunganisha ardhi walizoziteka huko Iraq na Syria ndiowaunde eneo moja wanalolitaja kama 'Islamic Caliphate' litakalotawaliwa na sheria kali za kiislamu, liwawatia tumbo joto mataifa mengi ya mashariki ya kati na mataifa ya kizungu hasa Marekani.Kwa kipindi cha mda mfupi ISIS imeweza kushambulia na kuyateka maeneo makubwa kwa kasi iliyowashangaza wengi huku serikaliza nchi husika zikishindwa kukabiliana nao.Kuzuka kwa kundi hili kunaleta tishojipya katika mashariki ya kati ambayo tayari inayumbishwa na vita na vizozo mbalimbali
KITUO CHA BOKO HARAM CHA SHAMBULIWA.. Jeshi la Nigeria limesema kuwa limekishambulia kituo cha ujasusi cha wapiganaji wa Boko Haram kinachodaiwa kuhusika na utekaji wa wasichana zaidi ya 200 nchini humo.Hata hivyo taarifa za jeshi hilo zinasema kuwa kiongozi wa kituo hicho cha Boko Haram Babuji Ya'ariamekamatwa.Ya'ari pamoja na kutuhumiwa kuhusika katika utekaji wa wasichana hao lakini pia alihusika katika mauaji ya kiongozi wa kijadi wa Gwoza, imebainisha taarifa ya serikali.Jishi hilo pia limegundua kuwa Ya'ari aliyekuwa mfanya biashara alikuwa akijifanya ni mwanaharakatikatika kutokomeza kundi la Boko Haram ili kupata nafasi ya kuchunguza harakati za jeshi la Nigeria na mipango dhidi ya kundi hilo la kigaidi.Anatuhumiwa kuhusika katika maandalizi ya mashambulio kadhaalikiwemo lile lililotokea Maiduguri na makao makuu ya mji wa Borno mwaka 2011.
FACEBOOK YALAUMIWA NA WATUMIAJI Mtandao wa Facebook umelaumiwakwa kuwafanyia wateja wake utafiti wa kisaikolojia bila ya kuwajulisha.Nia ya utafiti huo ilikuwa kujua kama wateja wake wamebadili tabiaya kuweka picha na mawazo yao katika mtandao huo kutokana na kukasirishwa na tabia za baadhi ya watumiaji wenzao.Utafiti huo uliohusisha takribani watumiaji 700,000 unaonyesha kuwa Facebook inacheza na taarifa za watumiaji wake ili kupata hisia zao katika kile wanachokiweka kwenye mtandao huo.Hata hivyo mtandao wa Facebook umekanusha madai hayo na kwamba hakuna mtumiaji binafsi aliyelengwa na utafiti huo uliofanywa na mtandao huo kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Cornell na California.“Ngoja tuuite utafiti kama Facebook wenyewe wanavyouita, lakini ni dalili za wazi za kushindwa kuzingatia maadili na nguvu ya kulinda haki za watumiaji wake” amesema Kate Crawford katika ukurasa wake wa Twitter.Waziri wa kazi Jim Sheridan mjumbe wa bodi ya mawasiliano ameagiza uchunguzi kufanyikadhidi ya mtandao huo wa Facebook katikatuhuma hizi.Hata hivyo Katherine Sledge Moore,Profesa wa Saikolojia katika chuo cha Elmhurst , Illinois amesema kwa jinsi ambavyo Facebook wamekuwa wakishughulika na taarifa za wateja wake makubaliano yaliyopo katika utafiti huo hadhani kama yapo nje ya hali ya kawaida.Adam Kramer kutoka Facebook mmoja kati ya walioandaa taarifa yautafiti huo anasema wanadhani kuwa ilikuwa mhimu kwao kutafiti mashaka yanayowakumba watumiaji hasa katika mawazo yanayowekwa na marafiki zao na jinsi yanavyowafanya wafikirie tofauti .
Jumapili, 29 Juni 2014
DIAMONDI ASEMA YAKE BAADA YA KUKOSA TUNZO ZA BET.... Tusipopenda kukubali Matokeo na Ushindi wa Wenzetu basi Daima Hatutaweza kuwa Washindani....Muhimu ni kujua wapi tulipotoka na Wapi tulipo Leo... Katika Nchi zaidi ya 20 zenye wasanii zaidi ya Million 40, kuchaguliwa Tanzania ni fursa, Heshima na Hatua kubwa... Cha Muhimu ni kuitumia vyema Fursa Hii na Kuhakikisha Mwakani tunapiga Hatua Zaidi!.... Asante sana kwa wote wanaozidi kuni support kwa hali na Mali, Mapambano ndio kwaaaanza yanaanza sasa.....!!!!!!@wcb_wasafiFor Life Baby ������
Jumamosi, 28 Juni 2014
Mubarak BalaMwanamume mmoja katika jimbo la Kano, nchini Nigeria, amepelekwa katika kituo cha matibabu ya kiakili baada ya kusema kuwa hamwamini Mungu.Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika moja lisilo la kiserikali nchini nIGERIA.Mubarak Bala alizuiliwa kinyume namatakwa yake hospitalini baada ya familia yake kumpeleka huko kwa matibabu.Duru katika hospitali hiyo zimesemakuwa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 29 alitibiwa kwa matatizo ya kiakili na kwamba hataendelea kuzuilikwa kwa muda mrefu.Jimbo la Kano lina idadi kubwa ya waumini wa kiisilamu, na limekuwa chini ya sheria za kiisilamu tangu mwaka 2000.Kano ni jimbo lenye kufuata sheria za kiisilamuShirika hilo la kimataifa limesema kuwa wakati ambapo Bala aliwaambia jamaa wake kuwa hamuamini Mungu, familia yake uilimpekeka kwa daktari kuuliza ikiwa akili yake iko timamu.Licha ya kufahamishwa kuwa mwanamume huyo hana tatizo lolote la kiakili, familia ya Bala ilitafuta ushauri wa daktari mwingine aliyewafahamisha kuwa hatua yake ya kumkana Mungu, inatokana na matatizo ya kiakili.Bwana Bala, ambaye ni mwanafunziwa chuo kikuu, alilazimishwa kupataushauri wa daktari wa kiakili , ingawa alitumia simu kuwasiliana na wanaharakati wa haki za kibinadamu.Hospitali ambako alikuwa ana pokea matibabu ilisema katika taarifa yake kuwa Bwana Bala hana tatizo lolote la kiakili na kuwa yuko sawa.Alilazwa hospitalini kwa sababu alihitaji kuchunguwa na daktari, ilisema taarifa ya hospitali hiyo.Taarifa zinazohusiana
Ijumaa, 27 Juni 2014
SALIM KIKEKE MTANGAZAJI WA HABARI IDHAA YA KISWAHILI ya BBC ametwaa taji la Mtangazaji wa Runinga Anayependwa katika toleo la kwanza laTuzo za Watu za Tanzaniaau Tanzania People’s Choice Awards katika sherehe zilizofanyika SerenaHotel, Ijumaa jijini Dar Es Salaam.Vipengele 11 (kumi na kimoja) vilikuwa vikishindaniwa. Mshindi katika kila kipengele ameibuka na zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na tuzo. Chini ya orodha ni picha za tukio hilo.ORODHA YA WASHINDI1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWAMillard Ayo – Clouds FM2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWAAmplifaya – Clouds FM3.MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWASalim Kikeke – BBC Swahili4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWAMkasi – EATV5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWAJuma Kaseja – Yanga6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWANisher7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWAYA MWANAMUZIKI WA KIUMEMy Number One – Diamond8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWAYA MWANAMUZIKI WA KIKEYahaya – Lady Jaydee09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWAKing Majuto10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWAElizabeth ‘Lulu’ Michael11. FILAMU INAYOPENDWANdoa YanguSalim Kikeke wa BBC Dira ya Dunia, mshindi wa kipengele cha Mtangazaji wa Runinga Anayependwa, akizungumza machache baada ya kutangazwa.
DADA(18) ASABABISHA AJALI 150 KWENYE MIKOA MBALIMBALI YA TANZANIA AKITUMIWA KICHAWI.HAYO YAMEJIZIHIRISHA BAADA YA MAOMBEZI YA SIKU SABA ZA UPONYAJI.ZIKIENDESHWA NA MWINJILIST EZEKIEL THOBIAS NYANGASI MKOANI MOROGORO.DADA HUYU ALIFUNDISHWA UCHAWI NA BIBI YAKE MZAA BABA AKIWA NA UMRI WA MIAKA KUMI.LAKINI BAADA YA MAOMBEZI HAYO ALIYO EDESHWA NA MWINJILIST THOBIAS NYANGAS DADA HUYO ALIFUNGULIWA KWENYE KIFUNGO HICHO CHA SHETANI.INAWEZEKANA NAWE UPO KATIKA VIFINGO MBALI MBALI KAMA MAGONJWA,KUOTA NDOTO MBAYA,KUKOSA KIBARI KATIKA KAZI ZAKO,MAFARAKANO KATIKA NDOA,KUIBIWA UFAHAMU KAZINI HILI UFUKUZWE KAZI,UMASIKINI .NK.MUNGU ATAKUWEKA HURU KUPITIA MTUMISHI EZEKIL THOBIAS 'YANGASI.KAMA UNAMATATIZO KAMA HAYO AU ZAIDI YA HAYO WASILIANA NA MTUMISHI WA MUNGU NO...+255757798093 OR..+255713110619.UKIONA NO ZIKO BUSY SUBIRI.MUNGU AKUBARIKI SANA..UPATAPO TANGAZO HILI MJULISHE NA MWEZAKO MWENYE MATATIZO HAYO.AMINA
Mashabiki wa Luis Suarez wakiwa uwanja wa ndege kumpokea mshambuliaji wao.MASHABIKI wa Luis Suarez wamefurika katika uwanja wa ndegewa kimataifa wa Carrasco karibu na Montevideo kumsalimia mshambuliaji huyo aliyerejea Uruguay baada ya kufungiwa na FIFA.Baada ya kufungiwa mechi tisa za kimataifa na miezi minne ya kutojihusisha na soka, Suarez amerejea Uruguay na kukiacha kikosi cha nchi yake kinachoshiriki kombe la dunia nchini Brazil.Mashabiki walilazimika kwenda uwanjani kumsalimia mshambuliaji huyo wa Liverpool.Rais wa Urugauy, Jose Mujica alikuwepo uwanja wa ndege tayari kumpokea nyota huyo, lakini aliondoka baada ya ndege ya Suarezkuchelewa kutua uwanjani.Shujaa: Mashabiki walifurika na kuziba njia ya uwanja wa ndege wa Carrasco wakisubiri kuwasili kwa Suarez.Vijembe: Shabiki akionesha ujumbe uliokusudia kuwasema FIFA baada ya kumfungia SuarezMashabiki walijikusanya uwanja wa ndege kumsalimia SuarezUruguay watachuana na Colombia katika mchezo wa hatua ya 16, lakiniwatahitaja ushindi bila ya Suarez pamoja na mechi nyingine zote watakazobahatika kucheza.Mshambuliaji wa Uruguay, Suarez akiwa katika hoteli ya timu yake ya Taifa nchini Brazil jana alhamisi.-
Rais wa Marekani, Barrack Obama ameliomba Bunge la Congress kiasi cha dola milioni mia tano kwa ajili ya kugharamia mafunzo na kuwapatia silaha Waasi wa Syria.Bado haijajuliakana ni aina gani ya msaada wa kijeshi ambao Marekaniitautoa japo kulikuwa na maombi yawaasi hao wa Syria kuhusu kupewa makombora ya kubeba ya kutungulia ndege ambayo yalitupiliwa mbali kwa kuhofia silaha hizo zisiwaendee wanamgambo wa makundi ya kigaidi.Ikiwa Bunge hilo litaridhia Ombi la Rais Obama,hii itakuwa mara ya kwanza kwa Jeshi la Marekani kujihusisha moja kwa moja kwenye mgogoro wa Syria, mashirika ya kiintelijensia ya Marekani tayari yanawasaidia waasi nchini Syria.Waasi wa Syria wanapambana na wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa ISIS, ambalo ni kundi la waislamu ambao pia wameteka mpaka ndani ya nchi ya Iraq.
Mwanamke wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa madai ya kuasi dini ya kiislam ameachiliwa huru baada ya kushikiliwa kwa mara ya pili.Meriam Ibrahimu alikwenda katika ubalozi wa Marekani uliyopo mji Mkuu wa Khartoum.Mumewe ana asili ya Sudan Kusini lakini kwa sasa ni raia wa Marekani.Mwanamke huyo aliachiliwa baada ya kuhukumiwa adhabu ya kifo siku ya jumatatu lakini alishikiliwa tena na polisi kwa tuhuma za kughudhi hati za kusafiria ili aondoke nchini Sudan kwenda Marekani.Kufuatia kuachiliwa huru kwa mara nyingine, Mke huyo wa Ibrahim ameiambia BBC kwamba ataendelea kuwa Mkristo.Kesi yake ya kuasi dini imevuta hisiaza watu wengi wakiwemo watetezi wa haki za binadamu pamoja na nchi za Magharibi.
Alhamisi, 26 Juni 2014
Jumatano, 25 Juni 2014
Wakazi wa sinza uzuri jijini Dar es salaam wamepigwa na butwaa baada ya kuona nyoka aina ya chatu anayedaiwa kutupwa katika daraja,baada ya kusemekana kuwa kuna watu walioiba sanduku wakidhani lina fedha ndani yake na walipofungua wakakutana na joka aina ya chatu ndani yake na kutelekeza sanduku hilo na kukimbia kusiko julika
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu wawili wanaoshukiwa kuwa majambazi ambao walikutwa wakiwa na bunduki mbili aina ya shortgun zikiwa zimekamatwa vitako huku moja ikiwa imefungiwa hirizi kama kinga ya kuzuia wasikamatwe katika matukio ya uhalifu. Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Bw Robert Boaz amesema, watu hao Ibrahimu Machaku na Laurenti Massawe wamekamatwa juzi na jana katika oparesheni maalum ya kupambana na matukio ya uhalifu ambapo pia walifanikiwa kukamata kilo 4.5 za dawa za kulevya aina ya Cocain kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro. Kamanda Boaz amewaambia waandishi wa habari kuwa Massawe ambaye ni mkazi wa Arusha pia alikamatwa akiwa na vitu vya dhahabu na simu mbili ambavyo aliporwa mfanyabiashara mmoja mjini Moshi Bw Mehboob Sadiki baada ya kuvunjwa nyumba yake Juni 22. Amesema, katika oparesheni hiyo polisi walikamata dawa hizo zikiwa zimetelekezwa na abiria aliyekuwa akisafiri na ndege kutoka Brazil kupitia Ethiopia, Mombasa hadi kwenye uwanja huo na jeshi la polisi limeanza kumsaka abiria huyo ambaye alitoweka
- Ni sehemu ya wengine 338 waoozea jela Vijana 65 wa Tanzania wamehukumiwa adhabu ya kifo nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Vijana hao ni kati ya zaidi ya 403 wa Tanzania wanaoshikiliwa katika nchi mbalimbali duniani kwa tuhuma ya kujihusisha na biashara hizo. Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, mjini Dodoma wakati akizungumzia Maadhimisho ya Siku Dawa za Kulevya Duniani yanayofanyika Juni 26 kila mwaka. Lukuvi alisema kuwa kwa mwaka huu maadhimisho hayo ya kesho, kitaifa yatafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nzovwe jijini Mbeya na Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. “Tangu mwaka 2008 kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wenye asili ya Kitanzania kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi, mpaka hivi sasa idadi yao ni kubwa kiasi cha kufikia zaidi ya 400, na wanashikiliwa katika nchi mbalimbali ambazo pia adhabu zao zinatofautiana kulingana na sheria za nchi hizo,”alisema Lukuvi. NCHI WANAKOSHIKILIWA Alizitaja baadhi ya nchi ambako vijana hao wanashikiliwa kuwa ni Brazil (108), Hong Kong (118), Kenya (34), Pakistan (16) na China 65. Nyingine ni Japan (7), Malawi (5), Uganda (3), Uswisi (2), Marekani (2), Uturuki (1), Botswana (5) na Msumbiji (1). “Orodha ya nchi waliko vijana hao ni defu zaidi,”alisema. Akizungumzia maadhimisho hayo kwa nchini, Lukuvi alisema kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni‘Uteja wa dawa za kulevya unazuilika na kutibika, chukua hatua'. AlisemaTanzania imeendelea kuwa miongoni mwa nchi zenye tatizo kubwa la dawa za kulevya kulingana na takwimu za ukamataji wa dawa hizo. Kwa mujibu wa Lukuvi, kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu kiasi cha kilo 220 za dawa hizo aina ya Heroine na watuhumwa 18 walikamatwa huku pia kilo 15.4 za Cocaine zilikamatwa na watuhumiwa saba. Lukuvi alisema kwa sasa dawa za kulevya ni tishio kubwa kwa maendeleo ya taifa kwa sababu imethibitika kuwa matumizi yake hupunguza tija na ufanisi wa nguvu kazi ya taifa. SHERIA MPYA YAJA Alisema katika kukabiliana na tatizo hilo, Serikali imekamilisha muswada wa sheria ya dawa za kulevya ambao kama utapitishwa bungeni na kuwa sheri kama ulivyo, unaweza kusaidia kwa Kiwango kikubwa kupunguza tatizo hilo. Lukuvi alisema tofauti na jinsi ilivyo sheria ya sasa, sheria mpya itaondoa adhabu ya faini na watuhumiwa kunyimwa dhamana wanapokamatwa, hali ambayo itasaidia kukabiliana na wasafirishaji na wauzaji wa dawa hizo. Kwa mujibu wa Lukuvi, sheria hiyo itakwenda sambamba na uundaji wa chombo imara cha kushughulikia dawa za kulevya ambacho kitakuwa na uwezo wa kupeleleza, kukamata na kushitaki watuhumiwa wa dawa za kulevya kama ilivyo kwa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Alisema kuwa muswada huo tayari umekamilika na kwamba wakati wowote unaweza kuwasilishwa bungeni ili upitishwe hatimaye kuwa sheria. Alisema maadhimisho hayo pia yatafanyika katika ngazi ya mkoa nchini na kuwaomba wananchi kujitokeza kushiriki ili waweze kupata elimu ya kutosha juu ya madhara na vita dhidi ya dawa hizo. KANDORO ANENA Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewataka wananchi mkoani mwake walioathirika na dawa za kulevya kujitokeza kwa wingi kupima afya zao, kupata tiba na ushauri katika maadhimisho hayo. Kandoro alifafanua kuwa maadhimisho hayo yanafanyika mkoani humo kutokana na takwimu kuonyesha una kiwango kikubwa cha tatizo la dawa za kulevya kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na kutoa mfano wa bangi ambayo inalimwa kwa wingi. “Kama mnavyojua, mkoa wetu upo mpakani hivyo tuna changamoto kubwa sana ya uingizaji wa dawa hizi, mara nyingi watu hukamatwa katika mipaka ya Tunduma na Kasumulo, hivyo ni budi elimu hii kutolewa kwa wananchi ili tushirikiane wote katika kutokomeza vita hii tuliyonayo,”alisema Kandoro. Alisema kuwa pombe aina ya viroba vya bei nafuu vitokavyo Malawi ni changamoto pia kwani vijana wengi wanavitumia, hivyo kuathirika kwa kiasi kikubwa.
JE DIAMOND ANGEFITI KUIMBA TAARABI....Msanii wa Bongo flava anaye-make headline ndani na nje ya TzeeDiamond Platnumzkwa sasa ana-hit na ngoma yakekali ya‘Mdogo Mdogo‘yenye mahadhi ya mchiriku baada ya ile iliyompa tuzo saba zaKTMA 2014.Katika moja ya mahojiano yaDiamond Platnumzna kituo cha redioClouds FMkupitia kipindi cha Hekaheka kinachoendeshwa na watangazaji mahiri kama Da Hu na Geah Habib aliweza kueleza kwamba kabla ajaanza kuimba muziki wa Bongo flava alikuwa anajifunza kuimba kwa kutumia muziki wa taarab kwa kutumia nyimbo za Mzee Yusuf na marehemu Omary Kopa na kitu kilichompelekea ku- apply kazi kwenye kundi la Jahaz Modern Taarab ili aweze kuimba taarab ” Unajua wakati najifunza kuimba nilikuwa najifgunza sana kupitia nyimbo za Mzee Yusuf na Marehemu Omary Kopa ili niweze kupanda na kushuka katika uimbaji wangu na ikanipelekea kwenda kuomba kazi Jahaz Modern Taarab ili niweze kujiunga kwenye kundi hilo.” alisema Diamond
Jumanne, 24 Juni 2014
TANESCO WATOA UFAFANUZI........kuhusiana na kukatika kwa umeme nchi nzima.Baada ya kukatika kwa umeme majira ya saa moja na dakika shirini na tatu na kusababisha karibu mikoa yote ambayo imeunganishwa na Gridi ya taifa kukosa nishati ya umeme na kusimamisha shughuli za bunge ikiwemo zoezi la upigaji wa kura ya bajeti ya serikali, mkurugenzi mtendaji wa shirika la umeme nchini Tanesco mhandisi FelchesimMramba ametoa afafanuzi juu ya kukatika huko kwa umeme na kubainisha kuwa mafundi wa shirika hilo wanaendelea kufanya uchunguzi nini kimesababisha tatizo la kukatika kwa umeme na kusababisha usumbufu kwa wateja.
Ijumaa, 20 Juni 2014
Jumatano, 18 Juni 2014
AZMA MPONDA MSANII WA MZIKI MWONDOKO WA HIP POP AKAMILISHA ALBAM YAKE YA LOVE STORIES YENYE NYIMBO 18 ZILIZO BEBA UJUMBE MZITO SO KWA YEYOTE ANAYE TAKA CD BASI AWASILIANE NA AZMA MPONDA YEYE MWENYE NA HAPO UTAPATA KUJUA MAMBO MBALI MBALI TOKA KWA MSANII HUYO WA MSIKI MIONDOKO YA HIP POP,NO YA SIMU NI 0712738888.
Jumatatu, 16 Juni 2014
ACHA KULIA SONG...ARTIST GAZUKO
Acha kuli ni wimbo unaogusa maisha ya watu wengi sana...kuna watu wanapitia mapito mbalimbali lakini Mungu akamtumia mwimbaji huyu kuwakomboa kutoka kwenye vifungo vyao kwa kuimba wimbo wa ACHA KULIA...
Video yake vile vile imesimama sana....Angalia utube andika ACHA KULIA GAZUKO...
ALOEVERA GEL NI DAWA YA VIDONDA VYA TUMBO
Ni dawa ya vidonda vya tumbo inayo tibu kwa haraka sana...Imetengenezwa kwa mimea ya alovevera haina kemikali yeyote.Inatibu kwa araka sana....Matumizi yake ni rahisi sana.Mimi nimetumia nimepona napenda na wewe utumie ili upone.....Kama unaitaji au ushauri wasiliana nasi nakupitia simu ya mkononi no 0714109277....
CPWAA AITINGISHA LINDI KWA SHOW YA NGUVU, JIONEE MWENYEWE HAPA

Msanii wa Kizazi kipya Nchini Tanzania Cp au unaweza mwita CPWAA
ameweza Kuandika historia katika Mji wa Lindi kwa kukonga nyoyo za
mashabiki wake katika Show kubwa na yanguvu aliyoitoa hapo Jana katika
Club Kubwa na yakipekee Mkoani Humu "Paric Club", Pia
Msanii huyo Clunk Master aliweza kuuza albam yake ambayo iko katika
mfumo wa CD kwa bei ya kawaida kabisa ikiwa ni zawadi kwa mashabiki wake
waliojitokeza kushuhudia show hiyo ambayo Ilikuwa ni yamfano na
haijawahi kutokea Mkoani humo.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)