Jumatano, 25 Juni 2014
JE DIAMOND ANGEFITI KUIMBA TAARABI....Msanii wa Bongo flava anaye-make headline ndani na nje ya TzeeDiamond Platnumzkwa sasa ana-hit na ngoma yakekali ya‘Mdogo Mdogo‘yenye mahadhi ya mchiriku baada ya ile iliyompa tuzo saba zaKTMA 2014.Katika moja ya mahojiano yaDiamond Platnumzna kituo cha redioClouds FMkupitia kipindi cha Hekaheka kinachoendeshwa na watangazaji mahiri kama Da Hu na Geah Habib aliweza kueleza kwamba kabla ajaanza kuimba muziki wa Bongo flava alikuwa anajifunza kuimba kwa kutumia muziki wa taarab kwa kutumia nyimbo za Mzee Yusuf na marehemu Omary Kopa na kitu kilichompelekea ku- apply kazi kwenye kundi la Jahaz Modern Taarab ili aweze kuimba taarab ” Unajua wakati najifunza kuimba nilikuwa najifgunza sana kupitia nyimbo za Mzee Yusuf na Marehemu Omary Kopa ili niweze kupanda na kushuka katika uimbaji wangu na ikanipelekea kwenda kuomba kazi Jahaz Modern Taarab ili niweze kujiunga kwenye kundi hilo.” alisema Diamond
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni