Jumatatu, 30 Juni 2014

KITUO CHA BOKO HARAM CHA SHAMBULIWA.. Jeshi la Nigeria limesema kuwa limekishambulia kituo cha ujasusi cha wapiganaji wa Boko Haram kinachodaiwa kuhusika na utekaji wa wasichana zaidi ya 200 nchini humo.Hata hivyo taarifa za jeshi hilo zinasema kuwa kiongozi wa kituo hicho cha Boko Haram Babuji Ya'ariamekamatwa.Ya'ari pamoja na kutuhumiwa kuhusika katika utekaji wa wasichana hao lakini pia alihusika katika mauaji ya kiongozi wa kijadi wa Gwoza, imebainisha taarifa ya serikali.Jishi hilo pia limegundua kuwa Ya'ari aliyekuwa mfanya biashara alikuwa akijifanya ni mwanaharakatikatika kutokomeza kundi la Boko Haram ili kupata nafasi ya kuchunguza harakati za jeshi la Nigeria na mipango dhidi ya kundi hilo la kigaidi.Anatuhumiwa kuhusika katika maandalizi ya mashambulio kadhaalikiwemo lile lililotokea Maiduguri na makao makuu ya mji wa Borno mwaka 2011.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni