Alhamisi, 24 Julai 2014
NDEGE YA ALGERIA YATOWEKA NA ABIRIA 116 Ndege ya Air Algerie imetoweka ikiwa na abiria 116Shirika la ndege la Algeria , Air Algerie, limesema kuwa limepoteza mawasiliano na moja ya ndege zakeilipokuwa ikitoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou.Afisa huyo anasema kuwa ndege hiyoya Air Algerie ilikuwa imepaa dakika 50 katika anga ya Sahara mara ya mwisho mawasiliano yao.Ndege hiyo iliokuwa inaeelekea mji mkuu wa Algiers, ilikuwa na watu mia na kumi na wahudumu sita .Oparesheni ya dharura ya kuitafuta ndege hiyo ieanzishwa,Ndege hiyo nambari AH 5017 inamilikiwa na shirika la ndege la kihispania la Swiftair.Mwandishi wa BBC Alex Duval Smith aliyeko katika mji mkuu wa Mali Bamako anasema kuwa kuna habari kuwa ndege hiyo huenda ilianguka katika eneo la janga la sahara kati yamji wa Gao and Tessalit .Mwandishi huyo wa BBC ananukuu ripoti kutoka kwa wanajeshi wa kulinda amani walioko huko Mali naduru za shirika la habari la AFP.Brigadia mkuu wa majeshi ya kulinda amani nchini Mali Koko Essien, amesema kuwa maeneo hayo ya jangwani yana idadi ndogo sana ya wakaazi kwa hivyo ni vigumu kupata habari kutoka huko na inawabidi kutafuta ilikoanguka ndege hiyo.Ndege ya Air Algerie imetoweka ikiwa na abiria 116Aidha Brig Essien anasema kuwa eneo hilo linamilikiwa na wapiganajiwaasi .Wamiliki wa ndege hiyo Swiftair wamesema kuwa ndege hiyo aina ya MD83 ilikuwa imeomba kubadili uelekeo wake kutokana na hali mbaya ya anga na ukungu mkubwa karibu na mpaka wa Algiers.Ndege namba AH 5017 husafiri kupitia njia ya Ouagadougou-Algiersmara nne kwa wiki,AFP imeripoti.Raia wa Algeria ni miongoni mwa abiria waliokuwa ndani ya Ndege hiyo,Gazeti moja la Algeria limeripoti.Mwezi Februari ndege ya kijeshi ya Algeria ilianguka na kuuwa watu 77 waliokuwemo.Tukio hili la hivi punde Linaloongezawasiwasi kuwa njia inayotumiwa na misafara ya ndege ziendazo sehemu hiyo inapitia eneo lenye utata la anga ya Mali.
Jumatano, 23 Julai 2014
AL SHABAB YAKIRI KUMUUWA MBUNGE NCHINI SOMALIA Mbunge wa Somalia Saado Ali Warsame amepigwa risasi na kuawa .Mwanamuziki mashuhuri ambaye pia mbunge katika bunge la SomaliaSaado Ali Warsame ameuawa kwa kupigwa risasi.Msemaji wa kundi la wanamgambo wa kiislamu al- Shabab Abdulaziz Abu Musab aliiambia BBC kuwa mbunge huyo aliauawa kutokana nasiasa zake wala sio muziki.Mwandishi wa bbc mjini Mogadishi Mohammed Moalimu anasema kuwa mbunge huyo ni wa nne kuawa mwaka huu.Bi Warsame alipata umaarufu wakati wa uongozi wa rais Siad Barre ambaye alipinduliwa mwaka 1991 kupitia nyimbo zake zilizokuwazikiiushutumu uongozi wake.Mbunge hiyo aliishi kwa kipindi kirefu nchini Marekani wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kabla ya kurejea nyumbani mwaka 2012 ili kuwakilisha ukoo wake kwenye bunge jipya nchini Somalia.Mapema mwezi huu mbunge mwengine Ahmed Mohamud Hayd aliuawa baada ya kutoka hotelini ambapo katika tukio hilo, mlinzi wake pia aliuawa na katibu wa Bunge pia alijeruhiwa .Mbunge wa Somalia Saado Ali Warsame amepigwa risasi na kuawa .Kundi la Al-Shabab, ambalo lina uhusiano na al-Qaeda, limeapa kuendelea na mashambulizi zaidi katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.Wanamgambo hao walipoteza ngome yao mjini Mogadishu na kuchukuliwa na Vikosi vya Umoja wa Afrika mwaka 2011,lakini wameendelea kutekeleza mashambulizi ya mabomu na mauaji mjini humo.Msemaji wa kundi hilo Abdulaziz Abu Musab amesema kuwa kundi lake limetekeleza mauaji kama ilivyopangwa na kuwa wataendelea kuwafuatilia Wabunge wengine ikiwa hawataachana na Bunge.Al-Shabab imekua ikipigania kuundataifa la kiislamu nchini Somalia.
Daktari aliyekua akiongoza mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone anapatiwa matibabu ili kupambana na Virusi vya ugonjwa huo, Taarifa kutoka Ofisi ya Rais imeeleza.Sheik Umar Khan alibainika kuwa naVirusi vya Ebola na sasa amelazwa katika hospitali moja mjini Kailahun ambapo ugonjwa huo umekua ukijitokeza kwa wingi.Zaidi ya Watu 630 wamepoteza maisha katika nchi tatu za Afrika magharibi tangu mlipuko wa ugonjwa huo kuanza nchini Guinea mwezi Februari, takwimu za Umoja wa Mataifa zimeonesha.Taarifa kutoka Ikulu ya nchi hiyo zimesema Waziri wa Afya alikua akibubujikwa na machozi aliposikia taarifa za dokta Khan.Ugonjwa wa Ebola umekua tishio katika ukanda wa Afrika magharibiWaziri wa Afya wa Sierra Leone Miatta Kargbo amemuita daktari huyo kuwa “shujaa wa taifa” na kusema kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha anapona.Mwandishi wa BBC wa mjini Freetown amesema wauguzi kadhaakatika hospitali ya Serikali mjini Kenema ambako kuna tishio kubwa la ugonjwa wa Ebola waligoma siku ya jumatatu baada ya wenzao watatu kupoteza maisha kwa kile kilichohisiwa kuwa ugonjwa wa Ebola.Mgomo huo ulisitishwa baada ya Serikali kusikiliza madai yao, ikiwemo kuhamisha wodi yenye wagonjwa wa Ebola kutoka hospitalina Operesheni ya kupambana na ugonjwa huo kuchukuliwa na Shirika la madaktari wasio na mipaka, Medicins Sans Frontieres.Jumamosi Shirika la afya duniani lilisema katika idadi ya 632 waliopoteza maisha Afika magharibikutokana na Ebola,watu 206 ni kutoka nchini SierraLeone
MBUNGE NA MWIMBAJI WA SOMALIA AUAWAMwanamuziki maarufu ambaye pia ni mbunge nchini Somalia, Saado Ali Warsame amepigwa risasi na kufa na wanamgambo.Aliuawa pamoja na mlinzi wake,katika shambulio la kutumia gari mjini Mogadishu. Msemaji wa kundi la al-Shabaab, Abdulaziz Abu Musab ameiambia BBC kuwa ameshambuliwa kutokana na sababu za kisiasa na sio muziki wake. Mwandishi wa BBC mjini Mogadishu Mohammed Moalimu amesema huyu ni mbunge wa nne kuuawa mwakahuu. Bi Warsame alipata umaarufu enzi za utawala wa rais wa zamani Siad Barre, aliyeondolewa madarakani mwaka 1991. Aliishi uhamishoninchini Marekani kwa muda mrefu na alirejea mwaka 2012 na kuwakilisha ukoo wake katikabunge jipya la Somalia. Mwandishi wa BBC Idhaa ya Kisomali Abdullahi Abdi anasema Bi Warsame atakumbukwa zaidi kwa muziki wake. Alikuwa mmoja wa wasomali wanawake wachache aliyepanda jukwaani bila kujifunika kichwa na mara nyingine kuvaa suruali, jambo ambalo sio la kawaida kwa wanawake wa Somalia, amesema Abdi.
AJALI YA NDEGE :MIILI IMEWASILI UHOLANZI Miili ya abiria wa ndege ya MalaysiaMH17 imewasili EindhovenNdege mbili za kijeshi zinazobeba miili 40 kati ya 282 ya abiria wale waliofariki kutokana na mkasa wa ndege ya Malaysia iliyodunguliwa huko mashariki mwa Ukraine , imewasili Uholanzi.Theluthi mbili ya waliofariki kwenye mkasa huo yaani 193 ni raia wa Uholanzi na nchi hiyo iko katika sikuya maombolezi ya kitaifa na bendereza ziko nusu mlingoti.Mfalme na malkia wa Uholanzi , waziri mkuu na viongozi wengine wako Eind-hoven pamoja na jamaa za waliouawa kupokea miili ya marehemu.Bado haijaeleweka ni miili mingapi kati ya ile wa watu 282 waliouawa , imefikishwa hapo jana.Miili ya abiria wa ndege ya MalaysiaMH17 imewasili EindhovenVifaa vya kurekodia mienendo ya ndege hiyo vimekabidhiwa wapepelezi wa Uingereza na maelezo kuvihusu yatakabidhiwa majajusi wa uholanzi .Maafisa wa kijasusi wa Marekani wamesema waasi wanaoiunga mkono Urusi waliitungua ndege hiyo kimakosa, lakini hakuna viashiria vyovyote kuhusu tukio hilo,vinavyohusiana moja kwa moja na Urusi.Waasi wameshutumiwa kuwakwamisha wapelelezi kwa kuwapa ushahidi wenye mashaka na kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusuidadi ya miili iliyopatikana.Katika hatua nyingine maafisa wa nchini Malaysia wamekabidhi kisanduku cheusi chenye kurekodi mawasiliano ndani ya ndege kwa mamlaka za uholanzi.
AJALI YA NDEGE :MIILI IMEWASILI UHOLANZI Miili ya abiria wa ndege ya MalaysiaMH17 imewasili EindhovenNdege mbili za kijeshi zinazobeba miili 40 kati ya 282 ya abiria wale waliofariki kutokana na mkasa wa ndege ya Malaysia iliyodunguliwa huko mashariki mwa Ukraine , imewasili Uholanzi.Theluthi mbili ya waliofariki kwenye mkasa huo yaani 193 ni raia wa Uholanzi na nchi hiyo iko katika sikuya maombolezi ya kitaifa na bendereza ziko nusu mlingoti.Mfalme na malkia wa Uholanzi , waziri mkuu na viongozi wengine wako Eind-hoven pamoja na jamaa za waliouawa kupokea miili ya marehemu.Bado haijaeleweka ni miili mingapi kati ya ile wa watu 282 waliouawa , imefikishwa hapo jana.Miili ya abiria wa ndege ya MalaysiaMH17 imewasili EindhovenVifaa vya kurekodia mienendo ya ndege hiyo vimekabidhiwa wapepelezi wa Uingereza na maelezo kuvihusu yatakabidhiwa majajusi wa uholanzi .Maafisa wa kijasusi wa Marekani wamesema waasi wanaoiunga mkono Urusi waliitungua ndege hiyo kimakosa, lakini hakuna viashiria vyovyote kuhusu tukio hilo,vinavyohusiana moja kwa moja na Urusi.Waasi wameshutumiwa kuwakwamisha wapelelezi kwa kuwapa ushahidi wenye mashaka na kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusuidadi ya miili iliyopatikana.Katika hatua nyingine maafisa wa nchini Malaysia wamekabidhi kisanduku cheusi chenye kurekodi mawasiliano ndani ya ndege kwa mamlaka za uholanzi.
Jumanne, 22 Julai 2014
KAMBI YA JESHI YAVAMIWA KINSASHA DRS Majeshi yazima shambulizi Kinshasa DRCKumetokea ufyatulianaji mkali wa risasi katika kambi ya kijeshi katika mji mkuu wa Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Taarifa zinasema kuwa raia wameondolewa katika eneo hilo na haijafahamika makabiliano hayo yaliyotokea katika kambi ya wanajeshi wa kumlinda rais yametokana na nini.Wadadisi wa mambo wanahisi kwamba kisa hiki huenda kikazusha utata tena kati ya Congo Kinshasa na Congo Brazzaville kwa vile shambulio lilitokea karibu na mpaka kati ya nchi hizo mbili.Taarifa kutoka kwa serikali zinasema kuwa wavamizi walijaribu kupenyeza katika kambi ya kijeshi yaCamp Tshatshi na makabiliano yalizuka kwa zaidi ya dakika 30 hivi.Jamhuri hiyo ya Kidemokrasia ya Congo imesakamwa na vita kwa kipindi kirefu sasa na hata rais aliyepo madarakani kwa sasa Joseph Kabila alichukua mamlaka baada ya kuuawa kwa babake Laurent Kabila mwaka wa , 2001.Majeshi yazima shambulizi Kinshasa DRCDuru zinasema kuwa wavamizi takriban 20 walijaribu kuingia ndaniya kambi hiyo lakini shambulizi likazimwa .Raiya walihamishwa kutoka maeneoyaliyoko karibu na uwanja wa ndegeulifungwa wakati wa shambulizi hilo.Serikali bado haijamtaja nani aliyeishambulia .Hii sio mara ya kwanza kwa Camp Tshatshi kushambuliwa mwaka uliyopita kami hiyo ilishambuliwa tena na wakati huo wafuasi wa dini ya ya kikristo ya dhehebu linaloongozwa na Paul Joseph Mukungubila walilaumiwa.
KAMBI YA JESHI YAVAMIWA KINSASHA DRS Majeshi yazima shambulizi Kinshasa DRCKumetokea ufyatulianaji mkali wa risasi katika kambi ya kijeshi katika mji mkuu wa Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Taarifa zinasema kuwa raia wameondolewa katika eneo hilo na haijafahamika makabiliano hayo yaliyotokea katika kambi ya wanajeshi wa kumlinda rais yametokana na nini.Wadadisi wa mambo wanahisi kwamba kisa hiki huenda kikazusha utata tena kati ya Congo Kinshasa na Congo Brazzaville kwa vile shambulio lilitokea karibu na mpaka kati ya nchi hizo mbili.Taarifa kutoka kwa serikali zinasema kuwa wavamizi walijaribu kupenyeza katika kambi ya kijeshi yaCamp Tshatshi na makabiliano yalizuka kwa zaidi ya dakika 30 hivi.Jamhuri hiyo ya Kidemokrasia ya Congo imesakamwa na vita kwa kipindi kirefu sasa na hata rais aliyepo madarakani kwa sasa Joseph Kabila alichukua mamlaka baada ya kuuawa kwa babake Laurent Kabila mwaka wa , 2001.Majeshi yazima shambulizi Kinshasa DRCDuru zinasema kuwa wavamizi takriban 20 walijaribu kuingia ndaniya kambi hiyo lakini shambulizi likazimwa .Raiya walihamishwa kutoka maeneoyaliyoko karibu na uwanja wa ndegeulifungwa wakati wa shambulizi hilo.Serikali bado haijamtaja nani aliyeishambulia .Hii sio mara ya kwanza kwa Camp Tshatshi kushambuliwa mwaka uliyopita kami hiyo ilishambuliwa tena na wakati huo wafuasi wa dini ya ya kikristo ya dhehebu linaloongozwa na Paul Joseph Mukungubila walilaumiwa.
SAKATA LA MIILI TANZANIA WANANE WAKAMATWA Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman KovaWatu wanane wanashikiliwa na polisi wakiwemo Madaktari kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio l a kutupwa kwa mabaki ya miili ya binadamu jana jioni nje kidogo ya jiji la DsmHuku likiendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo,Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova ametangaza kuundwa kwa jopo la upelelezi kuchunguza tukio hilo, ili kubaini taratibu gani zilikiukwa na kujua aina ya mashtaka itakayowakabili.Mabaki ya miili iliyotupwa eneo la Bunju Dar es SalaamUchunguzi wa awali umebainisha kuwa miili hiyo ilikua katika Taasisi ya mafunzo ya udaktari IMTU kabla ya kukutwa imetupwa eneo la Bunju.Taasisi hiyo imekiri kwamba mabakiya miili ilikua katika taasisi hiyo lakini haijatoa maelezo kuhusu kutupwa kwa miili hiyo.Kamanda Kova amewatoa wasiwasi watanzania kuwa hakuna mauaji yoyote ya kimbari yaliyotokea sehemu yeyote nchini hivyo polisi iachiwe ifanye kazi yake kisha itatoa taarifa hapo baadae.
VIUNGO VYA BINADAM VYAPATIKANA TANZANIA Viungo vya binadamu vikiwa vimefungwa mafurushiViungo mbali mbali vya binadamu vimekutwa katika eneo la kutupa taka la Bunju mjini Dar es Salaam katika mazingira ambayo haijafahamika mara moja kuwa viungo hivyo vimetoka wapi.Kwa mjibu wa Afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema viungo hivyo vya binadamu vilivyokutwa ni miguu,vidole ambavyo vilikutwa vikiwa vimefungwa ndani ya mifuko.Hata pamoja na viungo hivyo pia vifaa vya upasuaji vimekutwa zikiwemo glovuzi.Mtu mmoja anashikiliwa kuhusishwa na tukio hilo ambaye nidereva aliyekuwa akiendesha gari hilo lililobeba viungo hivyo vya binadamu.Haijafahamika mara moja miili hiyo ya binadamu imetolewa wapi na ilipelekwa eneo hilo kwa lengo gani.Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikikabiliwa na tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi au Albino ambapo viungo vyao huchukuliwa,japo kuwa viungo hivi vilivyokutwa kwa sasa bado havihusishwi moja kwa moja na matukio ya mashambulizi na mauajiya walemavu hao.
Jumapili, 20 Julai 2014
ALICHO SEMA KATULE WAKATI WA MAOJIANO NA BLOG HII
https://www.youtube.com/watch?v=R6Az2Jbf7xA&feature=youtube_gdata_player
Ijumaa, 18 Julai 2014
MSHITAKIWA WA UGAIDI MKENYA AKAMATWA TANZANIA Mmoja wa watuhumiwa wa matukioya ugaidi nchini Kenya,Jihad Gaibon Swaleh, amefikishwa mahakamani nchini Tanzania.Mshukiwa huyo amesomewa mashtaka ya kufadhili vitendo vya kigaidi nchini Kenya.Pamoja naye watuhumiwa wengine 16 ambao wanadaiwa kuendesha vitendo vya kigaidi nchini Tanzania pia wamefikishwa mahakamani hii leo wakikabiliwa na tuhuma za kula njama ya kutenda makosa ya kigaidinchini Tanzania.Washtakiwa wote 17 wamerejeshwarumande baada ya kusomewa mashtaka ya vitendo vya kigadi nchini Tanzania pamoja na nchi jirani ya Kenya.Upande wa mashtaka ukiongozwa na mwendesha mashtaka ambaye ni wakili wa serikali mwandamizi Prosper Mwangamila ulidai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kuwa kwa kutumia mtandao wa facebook aliweza kushawishi watu wengine kuwasiliana kwa lengo la kutafuta vifaa vya kulipua mabomu nchini Kenya na kusababisha majerahi, hofu na Vifo.Jihand Gaibon Swaleh ambaye amesomewa mashtaka mawili hakuruhusiwa kukiri wala kukana mashitaka yanayomkabili kutokana na kwamba mashitaka hayo yanaangukia katika makosa ya ugaidi ambayo kwa mujibu wa sheria nchini Tanzania mahakama ya Hakimu Mkazi haina mamlaka ya kuendesha kesi za namna hiyo.Katika kesi ya awali kutajwa mahakamani hapo washtakiwa wengine 16 walisomewa mashtaka mawili ikiwemo kula njama kutendakosa pamoja na kushawishi wenzao kushiriki katika vitendo vya kigaidi katika sehemu mbali mbali nchini Tanzania.Ni makosa ambayo wanadaiwa kutenda kati ya Januari mwaka 2013 na Juni 2014 katika maeneo tofauti Tanzania.Katika kesi zote mbili dhidi ya washtakiwa hao Upande wa mashtaka uliiambia mahakama iliyokuwa chini ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo bi Hellen Riwa kuwa upelelezi bado unaendelea na hivyo kuiomba mahakama kuahirisha kesi hizo hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Julai.Awali mapema asubuhi msemaji wajeshi la polisi nchini Tanzania Bi Advera John Bulimba aliwealeza waandishi wa habari kuhusu tuhuma dhidi ya washtakiwa haoHii ni mara ya kwanza kwa kundi kubwa la watuhumiwa kufikishwa mahakamani kwa pamoja wakikabiliwa na tuhuma za makosa ya kigaidi huku mtandao wa kijamii wa facebook nao ukitajwa kuhusika katika kutawanya taarifa za kuwezesha kutenda makosa hayo.Taarifa zinazohusiana
JESHI LA ARIDHI LA ISRAEL LAINGIA GAZA Sasa Israel yashambulia Gaza wakitumia vikosi vya angani, ardhinina majiniIsrael imeanzisha operesheni ya nchi kavu pamoja na mashambulizi ya anga na baharini dhidi ya vuguvugu la kupigania uhuruwa palestina Hamas katika ukanda wa Gaza.Katika kipindi cha siku kumi zilizopita zaidi ya wapalestina mia mbili wameuwawa katika mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na Israel na Muisraeli mmoja aliuwawa katika mashambulizi ya mizinga ya roketi kutoka Gaza.Oparesheni hiyo ya kupeleka majeshi ya ardhini imenza usiku, ni operation kubwa kufanywa katika kipindi cha miezi mitano.Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema lengo ni kuharibu kabisa miundo mbinu na silaha zinazotumiwa na vuguvugu laHamas kuishambulia Israel.Vifaru karibu kumi vimeshuhudiwa vikielekezwa Gaza huku mashambulio ya angani na majini yakiendelea, ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema huenda hata hospitali zimegwa na mizinga.Raia wa Gaza walia wakisema hamna pakutorokea huku mashambulizi ya Israel yakiongezekaWatu zaidi ya 3 wamefariki katika duru hii ya mapigano mbali na walezaidi ya 200 waliofariki awali.Kundi la Hamas limesema watajibu oparesheni hiyo vilivyo lakini Israel inasema Hamas watapewa kipigo cha kudumu na kitakachowasambaratisha kabisa.Israel imewaita maelfu ya wanajeshi wake wa akiba kuweka nguvu zaidi katika operation hiyo.Jana jamii ya kimataifa ilikuwa na matumaini makubwa kwamba huenda kukawa na usitishwaji mapigano wa kudumu baada pandezote mbili kukubali mapendekezo yakusitisha mapigano kwa mda wa saa 5 za kuruhusu huduma za kibinadamu.
NDEGE YA MALAYSIA YADUNGULIWA ABIRIA WOTE WAPOTEZA MAISHA Ndege hii ilikuwa inatoka Amsterdam kuelekea Kualar LumpurMaafisa nchini Ukraine wanasema kuwa ndege ya abiria iliyoanguka nchini humo ilidunguliwa katika eneo la mashariki mwa taifa hilo ambako waasi wanaoiunga mkono Urusi wamekuwa wakipigana na vikosi vya serikali.Wanasema abiria wote 298 waliokuwa katika ndege hiyo ya shirika la Malaysia iliyokuwa ikisafiri kutoka Amsterdam kuelekeaKualar Lumpur wamefariki.Wengi wa abiria hao walikuwa ni raia wa Uholanzi.Rais wa Ukraine Petro Poroshenko alitaja tukio hilo kama kitendo cha ugaidi.Maafisa wa Ukraine walichapisha kile walichotaja kuwa mawasiliano ya simu yaliyonaswa kati ya waasi wakiwaeleza maafisa wa Urusi kwamba ni wao ndio waliohusika katika kuindungua ndege hiyo.Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Ukraine, Pavlo Klimkin, amesema kuwa serikali ina ushahidiwa kutosha kwamba ndege hiyo ilidunguliwa.'Je waasi walihusika?''Tulinasa pia mawasiliano ya simu kati ya magaidi hao wakizungumzia kundunguliwa kwa ndege hiyo.Kwa sasa tunatafsiri sauti zao na kisha tutaziweka kwenye mtandao wa internet ili kuthibitisha hilo."Mabaki ya ndege ya Malaysia iliyodunguliwaHata hivyo sauti hizo zilizonaswa bado hazijathibitishwa na upande uliohuru na waasi hao wamekanusha kuhusika wakisema kuwa ni wanajeshi wa serikali ndio walioidungua ndege hiyo.Kadhalika marekani imesema kuwa inaamini ndege hiyo ililipuliwa angani na wala halikuwa tukio la ajali.Makamu wa rais Joe Biden hata hivyo amesisitiza kuwa Marekani bado inatafuta maelezo.''Ndege ya Malaysia iliyokuwa ikitoka Ulaya magharibi kuelekea Kuala Lumpur, yaelekea ilipokuwa ikivuka karibu na mpaka kati ya Ukraine na Urusi, nasema yaelekea kwa sababu hatuna taarifa za kina, nataka kuwa makini na kile ninachosema yaelekea ilidunguliwa,ilidunguliwa na wala sio ajali. Ililipuliwa kutoka angani. Tunaona ripoti kwamba huenda raia wa Marekani walikuwa kwenye ndege hiyo na bila shaka huo ndio wasiwasi wetu wa kwanza.''Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amesema kuwa Ukraine inapaswa kuwajibika katika tukio la udunguaji wa ndege hiyo.Msemaji wa serikali ya Urusi amesema kuwa mkasa huo haungetokea ikiwa Kiev haingeimarisha harakati zake za kijeshi mashariki mwa Ukraine.
WANAKIJIJI WATAKA BANGI IHALALISHWE MAKETE TZ Watu wa Makete hutumia mbegu zaMarijuana kukaangia chakula tangu zamaniHuku harakati za kutaka matumizi ya Bangi kuhalalishwa zikishika kasi katika sehemu mbali mbali duniani, Tanzania haijaachwa nyuma.Wanakijiji katika wilaya ya Makete , mkoa wa Njombe Kusini Magharibi mwa Tanzania wanataka serikali iweke sheria ambayo itaweza kuhalalisha matumizi ya mmea huo.Wanakijiji hao zamani walikuwa wakitumia mbegu za mmea huo kukaanga na chakula lakini siku hizi wanalazimika kuzitumia kwa usiri mkubwa wakihofia kukamatwa na polisi.Mwenyeketi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Daniel Okoka amesema matumizi ya Bangi katika wilaya hiyo hayajaanza leo, tangu zamani watu kitamaduni walikuwa wakitumia Mbegu za Bangi kukaanga na chakula.Na kama mmea huo ungekuwa na tahri kubwa kiafya, basi watu wengi wilayani humo wangekuwa vichaa.Majimbo mengi nchini Marekani yemahalalisha utumiaji wa Marijuana kwa sababu za kujistareheshaMiti ya mimea hiyo pia ilikuwa ikitumiwa kutengeza kamba ambazoanasema zilikuwa za nguvu sana.Lakini kwa sababu ya sheria kali, matumizi ya Bangi au Marijuana yanafanywa kichinichini katika wilaya hiyo.Mwandishi wa BBC Leonard Mubali,anaandaa taarifa hiyo huko wilayaniMakete na baadaye utaweza kuisikiliza katika redio na hapa kwenye mtandao.Lakini kwa sasa tunaulijza je ni ni sawa kwa Bangi kuhalalishwa kama chakula nchini Tanzania? toa maoni yako kwenye ukurasa wetu wa Facebook:
Alhamisi, 17 Julai 2014
TUNUSIA WAOMBOLEZA VIFO VYA WANAJESHI Jeshi la Tunisia likishika doria mpakaniTunisia imesema kuwa takriban wanajeshi wake 14 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa katika shambulizi la wanamgambo karibu na mpaka na Algeria.Maafisa wanasema wapiganaji waliojihami na makombora walishambulia vizuizi viwili vya kijeshi katika eneo la mlima Chaambi.Jeshi la Tunisia limekuwa likitekeleza oparesheni zake katika eneo hilo ili kujaribu kuwatimua wanamgambo wanaojificha katika eneo hilo.Inaarifiwa kuwa idadi kubwa ya vifo vya wanajeshi nchini humo tangu kujipatia uhuru mwaka 1956.Jeshi la Tunisia limekuwa likifanya operesheni dhidi ya wanamgambo, katika eneo hilo la milimani ,mwakajana.Wapiganaji wa kiisilamu wenye uhusiano na kundi la al-Qaeda, wanaaminika kujificha katika eneo la mpakani mwa nchi hiyo.Wanajesh hao, walishambuliwa na makundi ya wapiganaji Jumatano jioni walipokuwa wanafuturu.Kundi la wapiganaji lijulikanalo kama 'Okba Ben Nafaa Brigade' , limekiri kufanya mashambulizi hayokupitia ukurasa wao wa Facebook.Serikali imetangaza siku tatu za maombolezi, kuanzia leo Alhamisi.Wanajeshi wanane waliuawa katika shambulizi sawa na hili mwezi Julai mwaka 2013 , siku nyingi tu kabla yamauaji ya mwanasiasa Mohamed Brahmi, ambayo yaliitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro mpya wa kisiasa.
Ijumaa, 11 Julai 2014
ALIYE DHANIA KUPONA UKIMWI AUGUA TENA Virusi vya HIVMtoto mmoja nchini Marekani ambaye alidhaniwa kuwa mtu wa kwanza nchini humo kutibiwa virusi vya HIV akiwa mtoto, amepatikana tena kuwa na virusi hivyo.Mtoto huyo mwenye umri wa miakaminne kutoka jimbo la Mississipi amekuwa bila ya virusi hivyo kwa zaidi ya miaka miwili baada ya kupata matibabu maalum akiwa bado mtoto mdogo.Kisa chake kiliibua matumaini makubwa ya tiba ya ugonjwa wa ukimwi.Madaktari wanasema kuwa kuibuka tena kwa virusi hivyo kumewasikitisha sana.Madaktari walimpima mtoto huyo na kugundua kuwa angali ameambukizwa virusi vya HIV.Mwezi Machi mtoto huyo alipopimwa hakupatikana na virusi ikizingatiwa kuwa hakuwa anapokeamatibabu kwa karibu miaka miwili.Bila shaka taarifa hii ni pigo kwa matumaini ya matibabu kutoweza kumaliza virusi vya HIV mwilini kabisa.
Alhamisi, 10 Julai 2014
CHINA YAIPA SILAHA SUDANI KUSINI Sudan Kusini bado inakabiliwa na hali tete licha ya mkataba wa amani kutiwa sainiInaripotiwa kuwa China imetuma silaha zenye thamani ya dola milioni 38 nchini Sudan Kusini licha ya nchi hiyo kukabiliwa na mzozo ambao huenda utaitumbukiza katikabaa la njaa.Nyaraka zilizogunduliwa na wataalamu wa masuala ya ulinzi zinaonyesha kuwa makombora, bunduki za rashasha na risasi viliwasili nchini Sudan Kusini mweziuliopita kupitia bandari ya Mombasa nchini Kenya.Wanadiplomasia wanakadiria kuwa Sudan Kusini inatumia mamilioni yadola kwa ulinzi.Kwingineko, muungano wa ulaya umewawekea vikwazo viongozi na kupiga tanji mali ya wakuu wa kijeshi wa nchi hiyo kwa tuhuma za kukiuka makubaliano ya kusitisha vita ambayo yangeleta mazingira ya amani na kuziia mauaji ya maelfu yawanachi.Baraza la Muungano huo, halikuwataja wawili hao katika taarifa yao wala kutaja pande wanazounga mkono.Marekani imechukua hatua sawa nahizo dhidi ya viongozi kutoka pande zinazozozana.Vita vilizuka mjini Juba Disemba mwaka jana kati ya serikali na wapiganaji wa aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar.Mgogoro huo bila shaka umetonesha kidonda katika taifa hilo changa zaidi duniani tangu kujitawala mwaka 2011.Taarifa zinazohusiana
MIWANI INAYO WEZA KUSOMA MAWAZO YA MTU.. Miwani ya kisasa ya Google imedukuliwa, ambapo sasa inaweza kufanya kazi kwa kusoma mawazo ya mtu.Mtumiaji anaweza kupiga picha kwa kufikiria tu.Kwa kutumia miwani hiyo ya kisasa na kuunganisha kichwanina kifaa kijulikanacho kama electroencephalography (EEG) ambapo kifaa uroro huweza kusoma unachofikiria, na hata kupiga picha bila kujigusa au kubonyeza mahala popote.Kampuni ya This Place ya London iliyotengeneza kifaa uroro hicho (software) imesema inaweza kutumika pale watu wanapohitaji kufanya mambo mengine bila kutumia mikono yao, mathalan wakati madaktari wanafanya upasuaji.This Place imetoa kifaa uroro hicho MindRDR bure na wana imani kuwa huenda wataalam wengine wanaweza kutumia kwa shughuli nyingine.Hata hivyo Google imesema haitambui kifaa uroro hicho."Miwani yetu ya Google haiwezakusoma mawazo ya mtu" msemaji wa Google ameiambia BBC.Kutaka kujaribu kifaa uroro hicho kama una miwani ya
ISRAEL YAENDELEZA MASHAMBULIZI GAZA Zaidi ya watu sabini wameuawa Palestina tangu mzozo kuanza kati ya Israel na PalestinaNdege za Israel zimesababisha vifo vya wapalestina 9 waliokuwa wakitizama mchuano wa kombe la Dunia, ndani ya mgahawa mmoja katika mji wa Khan Yunis huko Gaza.Jumla ya watu 20 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na Israel dhidi ya wapalestina katika ukanda wa Gaza usiku kucha.Taarifa hii ni kwa mujibu wa maafisa wakuu wa kipalestina.Wizara ya afya imesema kuwa wengi walifariki katika mashambulizi yaliyofanywa dhidi yanyumba na mgahawa katika eneo laKhan Younis, Kusini mwa Palestina.Vifo hivyo vimefikisha idadi ya watu waliofariki hadi 76 upande wa wapalestina tangu vita kuanza kati ya pande hizo mbili.Wapiganaji katika ukanda wa Gaza waliendelea kurusha makombora nchini Israel Alhamisi usiku huku ving'oa vikisikika kila sehemu ya miji ya Kusini.Msemaji wa wa Israeli awali alisema kuwa vifo vya watu 8 siku ya Jumanne ilikuwa ajali tu na haikuwa nia ya Isarel kusababisha vifo hivyo.Israel bado haijatoa idadi ya watu wake waliofariki au kujeruhiwa lakini Palestina ingali inarusha makombora yake katika ardhi ya Israel.Huku hayo yakijiri, Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki-moon, ameonya kuwa hali huko Gaza imo ukingoni na huenda ikawa mbaya kiasi cha kutoweza kudhibitiwa.Ban amesema eneo hilo haliwezi kuhimili vita vingine huku akitoa wito kwa pande zote zisitishe ghasia.Amelitaka kundi la Hamas lisite kurusha makombora nchini Israel na ameiomba serikali ya Israel kujizuia na iheshimu jukumu lake la kimataifa ili kuwalinda raia.Israel says its targets have been militant fighters and facilities including rocket launchers, weapons stores, tunnels and command centres.'Tap on roof'The Israeli military saidthat it had attacked 108 targets since midnight and that 12 rockets had been fired at Israel, seven of them intercepted by the Iron Dome defence system.Palestinian sources say the cafe in Khan Younis was hit while people were watching the world cup semi-final on television. First reports say that nine people died in that attack.Separately, eight Palestinians were killed in an air strike on a house near the city, the Palestinian health ministry said.
Jumatano, 9 Julai 2014
UHARAMIA UENDA UKAPUNGU NCHINI SOMALIA Utafiti wa hivi karibuni unaashiria kwamba uharamia kutoka pwani ya Somalia huenda ukapungua kwa kiwango kikubwa kwa kuwapatia wazee wa koo za kisomali njia mbadala za kujikimu kimaisha.Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti huo wa chuo kikuu cha Oxford na King's College mjini London, iliyochapishwa katika jarida moja la Uingereza, Jamii huwalinda maharamia wakati hawana njia nyengne za kujipatia kipato.Kwa sasa Jamii ya kimataifa inategemea mikakati iliyo ghali mno, zikiwemo meli za kijeshi kuzuia uhaharamia wa majini na kuweka njia za safari za majini kuwasalama .Lakini utafiti huu unakubaliana na yale ambayo yamekuwa yakipendekezwa na wadau mbalimbali Afrika mashriki, kwamba suluhu la kudumu ni kujenga miundo mbinu kama vile bandari na barabara zitakazo wawezesha wanavijiji wa koo mbalimbali wanufaike kwa fursa za kibiashara halali, zitakazowawezesha kupata tiza za kuendeleza maisha yao.Watafiti wamebaini maeneo meli zilokotekwa nyara kote bahari ya SomaliaMwandishi wa utafiti huo anasema awali watunga sera wameazimia zaidi kutafuta kiini na vichochozi vyauharamia wa baharini pasi na kuchunguza ni kwa nini wanalindwana jamaa zao na viongozi wa mbari zao.Watafiti hao wameweza kubaini maeneo meli zilikotekwa nyara kote bahari ya Somalia, na wakitumia data walizozopata kutoka kwa Benki ya dunia , walifanya mahojiano na wakaazi wa sehemu hizo.Uharamia umekithiri katika maeneomaskiniIkabainika wazi kwamba uharamia umeenea zaidi katika maeneo ambayo yamefungiwa kufikia njia zabarabara za kibiashara hasa zinazoelekea bandarini, kwa mfano maeneo yanayozozaniwa huko Puntland na Somalia ya kati.Wakagundua pia kuwa katika yale maeneo ambako wakaazi wanaendendeleza biashara halali ama kwa kutoza kodi , kwa kuingiza au kuuza bidhaa nje ya nchi, kupitia bandarini kamwe hawamlindi haramia wa baharini.Katika maeneo maskini na vitongoji duni, ilionekana mtindo wa visa vya uharamia wa majini na utekaji nyara meli, kuongezeka kila wakati wa upigaji kura za mitaani humo, kumaanisha tabia hiyo si tofauti na za wanasiasa.Kwa mfano uitaliano na Taiwan walio na mtindo wa kuwalinda wahalifu kwa lengo la kupata fedha kwa njia haramu zitakazowanufaisha katika malengo yao ya kutwaa madaraka ya kisiasa.Mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo Federico Varese, kutoka chuo kikuu cha Oxford Uingereza amesema jamii hizo huwalinda maharamia wamajini wakati hamna namna nyengine ya mapato mazuri.Huku mwandishi Dr Anja Shortland,wa chuo kikuu cha Kings London, akajumuisha kuwa itabidi suluhu la uharamia wa majini lipatikane ardhini kwa maana kuwa kama vile benki ya Benki ya dunia inavyopendekeza, kuwe na mkatabawa kuweka mfumo thabiti wa kisiasa utakaofanikisha maendeleo ya kijamii. ..
FIFA IMEMPIGA MARUFUKU NIGERIA FIFA imeipiga marufuku NigeriaNigeria imepigwa marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya kandanda yanayoandaliwa na shirikisho la soka duniani FIFA.Hatua hii imeafikiwa baada ya maafisa wa serikali kuwaondoa wasimamizi wa shirikisho la soka nchini Nigeria NFF afisini.Marufuku hii inamaanisha hakuna klabu yeyoye ya soka nchini Nigeria inaweza kushiriki mashindano yeyote ya Kimataifa.FIFA ilikuwa imeionya Nigeria kuwa ingeichukulia hatua ifikiapo Jumanne kama Shirikisho la NFF halijarejeshewa madaraka yao lakini Serikali ikapuuza makataa hayo.Mwishoni mwa juma Serikali ya Nigeria ilikuwa imemteua afisa mshikilizi kuongoza shirikisho hilo hadi uchaguzi wa huru na wa haki utakapofanyika kulingana na taarifa ya wizara ya michezo.FIFA katika taarifa imeonya kuwa marufuku hiyo itaondolewa tu iwapo maafisa waliochaguliwa watarejeshwa mamlakani.Marufuku hiyo itaathiri timu ya taifaya Super Eaglets ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 20 ambayoinapaswa kushiriki mchuano wa kombe la dunia iwapo marufuku hiyo haitaondolewa ifikapo juma lijalo.(Julai15)FIFA imeipiga marufuku NigeriaMsemaji wa serikali hata hivyo alisema kuwa hatua iliyochukuliwa dhidi ya NFF ilifuata kanuni kwani hata kiongozi wa shirikisho la soka la Nigeria Aminu Maigari alikamatwa na polisi punde baada ya kurejea nyumbani kutoka Brazil.Mahakama ya Nigeria ilikuwa imeamua kuwa Maigiri hakuwa anastahili kuendelea kuiongoza NFF haswa baada ya matokeo duni hukoBrazil.Wajumbe wa NFF waliafiki kauli ya mahakama ya kumn'goa mwenyekitihuo madarakani lakini lakini kwa sasa erikali ya Nigeria inasubiri mawasiliano kutoka FIFA baada ya kutuma ithibati ya mkutano maalumuliofanyika na wajumbe wa shirikisho la soka la NFF .Mabingwa hao wa Afrika walishindwa katika mkondo wa pili wa kombe la dunia na Ufaransa .Hiyo ilikuwa ni mara ya tatu kwa timu hiyo kufuzu kwa mkondo wa pili baada ya kufuzu mwaka wa 1994na 1998.
MSTAKABALI WA SUDANI KUSINI Mbali na soka sasa...Sudan Kusini inaadhimisha miaka mitatu tangu kujipatia uhuru na kuwa nchi changa zaidi duniani kupata uhuru.......Tangu uhuru, migogoro imechacha, mauaji yameshuhudiwa kila kuchao na mapatano bado ni kama maji ya moto kwa viongozi wa nchi hiyo.Nani anaweza kunusuru Sudan Kusini?Nini unadhani kifanyike ili nchi hiyo ipateamani ya kudumu?
Jumanne, 8 Julai 2014
BANGI YAHALALISHWA WASHINGTON MAREKANI Bhangi ni halali katika majimbo 23 ya MarekaniMatumizi ya Bangi kwa ajili ya kujiburudisha yamehalalishwa katika jimbo la Washington nchini Marekani.Washington ni jimbo la pili nchini Marekani kuhalalisha Bangi , baada ya Colorado, ambako jimbo hilo linajipatia mamilioni ya dola kila mwezi kwa kutoza ushuru biashara za Bangi kwa wanaoitumia kujiburudisha.Hata hivyo utaratibu wa kuuza bidhaa hiyo utadhibitiwa ipasavyo katika jimbo hilo.Ni maduka 25 pekee yaliyoruhusiwakuuza Bangi hadi sasa, ingawa maafisa wanaamini kuwa idadi ya maduka huenda ikaongezaka na kufika miamoja.Katika sehemu zingine za Marekani, majimbo 23 yanaruhusu matumizi ya Bangi kwa sababu za kimatibabu.
WASHITAKIWA 2 WAKAMATWA NA POLICE ARUSHA TANZANIA Watu wawili wamekamatwa na Polisi wakihusishwa na shambulio la bomu lililotokea kwenye mgahawa wa 'Vama Traditional Indian cuisine' jijini Arusha Kaskazini mwa Tanzania.Shambulizi hilo liliyokea siku ya jumatatu saa nne usiku.Watu wasiojulikana walirusha bomundani ya mgahawa kupitia mlangoniambapo watu wanane wamejeruhiwa moja kati yao akiwa na majeraha makubwa.Aidha,katika matukio mengine, jumla ya Watu 20 wanazuiliwa na Polisi wakiwemo watu sita wanaosadikiwa kujihusisha na mlipuko wa bomu uliotokea mkoaniArusha juma lililopita nyumbani kwa Kiongozi wa dini Sheikh Sudi Ally Sudi na kujeruhi watu wawili.Polisi wanaendelea na upelelezi kuhakikisha inawatia nguvuni watu waliohusika na matukio hayo.Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo.
MAJAMBAZI WAVAMIA KIWANDA CHA SUMSUNG BRAZIL. Wezi waliiba simu 40,000 na tarakilishi pamoja na vifaa vingineWezi walivamia kiwanda cha simu cha Samsung nchini Brazil usiku wa Jumatatu na kuiba mali yenye thamani ya dola milioni thelathini na sita.Mali hiyo ilikuwa pamoja na simu zamkononi na komputa.Genge hilo lililokuwa limejihami vikali, liliwateka wafanyakazi wanane waliokuwa wanaodnoka kazini na kuiba vitambulisho vyao ambavyo walivitumia kuweza kuingia katika kiwanda hicho mjini Sao Paulo.Inaarifiwa wezi hao waliwazidi nguvu walinzi na kuchukua muda wa saa tatu kufanya wizi huo.Polisi wanasema kuwa genge hilo lilikuwa na wezi, 20 ambao walifanikiwa kuiba simu 40, 000 pamoja na tarakilishi, tabiti na vifaa ningine vyenye thamani ya dola milioni 36.Walipovamia kiwanda hicho waliamuru wafanyakazi wote kuondoa betri zao kwenye simu ili wasiweze kumpigia mtu yeyote simu.Walifanya wizi kiwandani kwa karibu masaa matatu na walifahamu vyema ambako vifaa vyenye thanai zaidi vilikuwa vimewekwa.Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa na kwamba kampuni hiyo haina tatizo lolote kwa sasa.Polisi wanachunguza kanda za videokuona ikiwa wanaweza kuwatambuawezi hao.
8 WAJERUHIWA KATIKA MLIPUKO MKOANI ARUSHA TZ.. Watu wanane wamejeruhiwa mmoja akiwa hali mahututi kufuatiamlipuko katika mkahawa mjini Arusha TanzaniaMlipuko huo ulitokea Jumatatu jioni na polisi wangali wanachunguza kilichousababisha.Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mlipuko huo ulitokea Jumatatu jioni na kuwajeruhi watu wanane huku mmoja akiwa hali mahututi.Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo.Kufika sasa afisaa mkuu wa shirika la ujasusi nchini humo anakutana na wandishi wa habari. Taarifa zaidipunde tutakapozipata.Taarifa zinazohusiana
Jumatatu, 7 Julai 2014
JE UNAIJUA SARAFU MPYA YA TANZANIA YA SHILINGI 500???HII HAPA ITATUMIKA HIVI KARIBUNI.. Sarafu ya Shilingi Mia Tano ambayoBenki Kuu ya Tanzania inatarajia kuitoa hivi karibuni. Noti ya Mia Tano maarufu kama 'Jelo' itaendelea kutumika, ila itaondolewa taratibu katika mzunguko, kwa mujibu waMkurugenziwaHuduma za Kibenki na Sarafu wa BoT,BwEmmanuel Boaz, aliyeiambia Globu ya Jamii kwenye banda la Benki Kuu katika Maonesho ya SabaSaba jijini Dar es salaam.
WANAWAKE 60 WAWAKWEPA BOKO HARAM NCHINI NIGERIA Wapiganaji wa Boko HaramTaarifa kutoka Kaskazini Mashariki mwa Nigeria zinasema kuwa zaidi ya wanawake 60 wakiwemo wasichana wa umri mdogo waliotekwa nyara mwezi jana na Boko Haram wamekwepa.Taarifa hii inakuja wakati sawa na taarifa za kutokea makabiliano makali kati ya jeshi la Nigeria na wapiganaji wa kundi hilo.Wanawake hao wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wanawake 68 waliotekwa nyara mwezi uliopita karibu na mji wa Damboa Kaskazni Mashariki mwa jimbo la Borno.Serikali ya Nigeria imeitisha uchunguzi wa kina juu ya namna walivyotoweka wasichana hao.Hali ya usama ani mbaya sana hukumiundo mbinu duni ikichangia kuifanya hali ngumu kuweza kufikia maficho ya kundi hilo na pia kubainiidadi ya wasichana waliotoroka kutoka mikononi mwa Boko Haram.BBC imeongea na jamaa ya wasichana watatu ambao walitoroka. Sasa wako salama nyumbani kwao na mmoja wao amesema kwamba wasichana wengi wamefanikiwa kutoroka.Baadhi ya vyombo vya habari nchinihumo vinadai kuwa huenda wasichana hao walitoroka siku ya Ijumaa, pale watekaji nyara walipokwenda kushamblia kambi yakijeshi.Maafisa wakuu hata hivyo bado hawajaweza kuthibitisha kukwepa kwa wasichana hao.Wakati huohuo hapajakuwa na taarifa zozote kuhusu wasichana 200 waliotekwa nyara katika shule ye mabweni ya Chibok mwezi Aprili.Hatua ambayo imekemewa vikali najamii ya kimataifa huku baadhi ya mataifa kama vile Marekani, Uingereza na hata Ufaransa wakijitolea kuisaidia serikali ya Nigeria kuwasaka wasichana hao.Taarifa zinazohusiana
Ijumaa, 4 Julai 2014
MAFUTA YA BENZI NA UMEME YAPANDA NCHINI MISRI Uhaba wa mafuta nchini MisriBei za mafuta na umeme zilizopanda zimeanza kutekelezwa nchini Misri huku serikali ikianza kukata ruzuku yake mbali na kupunguza matumizi ya bajeti yake ili kufufua uchumi ulioathiriwa na mgogoro wa kisiasa wa miaka kadhaa.Baadhi ya bei za mafuta zinadaiwa kupanda kwa asilimia 78 huku bei ya umeme ikipanda maradufu katika kipindi cha miaka mitano.Kwa sasa serikali inauza umeme kwa nusu ya gharama ya uzalishaji wake.Kukatika kwa umeme nchini Misri limekuwa jambo la kawaida na maafisa wanasema kuwa gharama ya juu ya ruzuku imelemaza ukarabati na upanuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme.Waandishi wanasema kuwa kupanda kwa bei ya umeme nchini humo ni hatua mojawapo ya serikali katika kile kinachotarajiwa kuwa marekebisho ya kisiasa kwa ruzuku zinazosimamia Mafuta,Uchukuzi,chakula na kilimo.Taarifa zinazohusiana
Jumatano, 2 Julai 2014
SERIKALI YASIBITISHA KIFO CHA BALOZI WA LIBYA TANZANIA... Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Assa Mwambene. Mwambene amesema mpaka sasa chanzo cha kifo cha balozi huyo hakijajulikana.Msemaji wa serikali hapa nchiniAssa Mwambene amekiri kutokea kwa kifo cha Balozi Msaidizi wa Libya nchini bwana Ismail Nwairat kwa kujipiga risasi mwenyewe majira ya saa saba usiku katika chumba cha ofisi za ubalozi huo.Mwambene alisema kuwa mpaka sasa haijafahamika kifo cha balozi huyo kimetokana na nini, ila wafanyakazi wa karibu katika ubalozi huo wamesema kuwa walisikia mlio wa risasi chumbani kwake, na walipojaribu kufungua mlango ulikuwa umefungwa na wakatumia nguvu ya kuvunja mlango huo na kufanikiwa kumkuta balozi yupo katika hali ya mbaya.Aidha walimuwahisha katika hospital ya Ami iliyopo Oysterbay na baada ya nusu saa madaktari walithibitisha kuwa amefarika dunia.Serikali imesikitishwa na kifo hicho na wanafanya utaratibu wote wa kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka nchini kwao kwa ajili ya mazishi.
NDEGE YA MIZIGO KENYA YAPATA AJALI.WATU WAPOTEZA MAISHA.Shughuli za uokozi zikiendelea baada ya ndege ya mizigo kuangukajijini NairobiWatu wanne akiwemo Rubani wa ndege moja ya mizigo, wamefariki dunia baada ya ndege walimokuwa kuanguka mapema leo asubuhi katika mtaa wa Embakasi jijini Nairobi.Kwa mjibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya, ndege hiyo ilianguka dakika chache tu baada ya kuruka kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.Ndege hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba shehena ya Miraa ama Mairungi kuelekea Mogadishu nchini Somalia.Uchunguzi umeonyesha kuwa ndege hiyo huenda iligonga mlingoti wa stima karibu na mtaa wa Embakasi, mjini Nairobi na kuanguka.
Jumanne, 1 Julai 2014
18 WAUWAWA BAADA YA KULIPUKA KWA BOMU NCHINI NIGERIA.. Uharibifu uliotokea baada ya shambuliziTakriban watu 18 wameripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea sokoni mjini Maiduguri Kaskazini mwa Nigeria.Watu walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC kuwa gari lililokuwa limebeba mkaa lilipuliwa na bomu linalodhaniwa liliwekwa ndani ya gari hilo.Hadi sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lililokiri kufanya shambulio hilo.Tukio hili linakuja huku ripoti ya hivikaribuni ya jeshi la Nigeria ikisema kuwa limeshambulia moja ya ngome za kundi la wapiganaji la Boko Haram.Boko Haram wamekuwa wakifanya mashambilizi ya mara kwa mara licha ya operesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji haoMwandishi wa BBC Habiba Adamu toka mji mkuu wa Nigeria Abuja aliyetembeela eneo hilo anasema kuna utata wa idadi ya waliouawa katika shambulio hilo kwani wakati wengine wakisema waliouawa ni watano wengine wanasema huendaidadi ya waliouawa ikawa ni zaidi yahiyo iliyotolewa.
MGOMO KWA MARA NYINGINE AFRICA YA KUSINI.. Wafanyakazi hawa wanataka nyongeza maradufu ya mishahara yaoWanachama wa chama kikubwa zaidi cha wafanyakazi Nchini Afrika Kusini watagoma wakidai mshaharawao kuongezwa kwa kiwango kikubwa.Wanachama hao wanataka mishara akuongezwa maradufu ya kiwango cha mfumo wa bei nchini humo.Chama cha kitaifa cha wafanyakazi wa Chuma na wahandisi kinanasema kuwa zaidi ya wanachama elfu 200 watashiriki mgomo huo.Watafanya maandamano katika mijisita muhimu nchini humo.Mgomo huo utakua pigo kubwa katika uchumi wa Afrika Kusini ambayo imekumbwa na migomo yawafanyikazi wa migodi na viwanda kwa miezi mitano iliyopita baada ya mgomo wa kampuni ya dhahabu nyeupe ulioisha juma lililopita.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)