Jumatano, 23 Julai 2014
AJALI YA NDEGE :MIILI IMEWASILI UHOLANZI Miili ya abiria wa ndege ya MalaysiaMH17 imewasili EindhovenNdege mbili za kijeshi zinazobeba miili 40 kati ya 282 ya abiria wale waliofariki kutokana na mkasa wa ndege ya Malaysia iliyodunguliwa huko mashariki mwa Ukraine , imewasili Uholanzi.Theluthi mbili ya waliofariki kwenye mkasa huo yaani 193 ni raia wa Uholanzi na nchi hiyo iko katika sikuya maombolezi ya kitaifa na bendereza ziko nusu mlingoti.Mfalme na malkia wa Uholanzi , waziri mkuu na viongozi wengine wako Eind-hoven pamoja na jamaa za waliouawa kupokea miili ya marehemu.Bado haijaeleweka ni miili mingapi kati ya ile wa watu 282 waliouawa , imefikishwa hapo jana.Miili ya abiria wa ndege ya MalaysiaMH17 imewasili EindhovenVifaa vya kurekodia mienendo ya ndege hiyo vimekabidhiwa wapepelezi wa Uingereza na maelezo kuvihusu yatakabidhiwa majajusi wa uholanzi .Maafisa wa kijasusi wa Marekani wamesema waasi wanaoiunga mkono Urusi waliitungua ndege hiyo kimakosa, lakini hakuna viashiria vyovyote kuhusu tukio hilo,vinavyohusiana moja kwa moja na Urusi.Waasi wameshutumiwa kuwakwamisha wapelelezi kwa kuwapa ushahidi wenye mashaka na kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusuidadi ya miili iliyopatikana.Katika hatua nyingine maafisa wa nchini Malaysia wamekabidhi kisanduku cheusi chenye kurekodi mawasiliano ndani ya ndege kwa mamlaka za uholanzi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni