Jumanne, 1 Julai 2014
18 WAUWAWA BAADA YA KULIPUKA KWA BOMU NCHINI NIGERIA.. Uharibifu uliotokea baada ya shambuliziTakriban watu 18 wameripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea sokoni mjini Maiduguri Kaskazini mwa Nigeria.Watu walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC kuwa gari lililokuwa limebeba mkaa lilipuliwa na bomu linalodhaniwa liliwekwa ndani ya gari hilo.Hadi sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lililokiri kufanya shambulio hilo.Tukio hili linakuja huku ripoti ya hivikaribuni ya jeshi la Nigeria ikisema kuwa limeshambulia moja ya ngome za kundi la wapiganaji la Boko Haram.Boko Haram wamekuwa wakifanya mashambilizi ya mara kwa mara licha ya operesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji haoMwandishi wa BBC Habiba Adamu toka mji mkuu wa Nigeria Abuja aliyetembeela eneo hilo anasema kuna utata wa idadi ya waliouawa katika shambulio hilo kwani wakati wengine wakisema waliouawa ni watano wengine wanasema huendaidadi ya waliouawa ikawa ni zaidi yahiyo iliyotolewa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni